Jumatano, 14 Novemba 2018

 

 

 

 

 

TAARIFA KWA UMMA

 

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), linapenda kuwakumbusha vijana wote walioteuliwa kujiunga na Mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2018 kuwa tarehe ya mwisho ya kuripoti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa ni tarehe 10 Juni 2018.

 

Aidha, JKT linasisitiza kuwa ni kosa la sheria kwa mhitimu yoyote wa elimu ya kidato cha sita aliyeteuliwa kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria (compulsory) na kukaidi kuhudhuria mafunzo hayo.

 

Kosa hilo ni kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha Jeshi la Kujenga Taifa nchini ya mwaka 1964 na kufanyiwa marejeo mwaka 2002.(The National Service Act [CAP 193 R.E. 2002].

 

Mkuu wa JKT anawakaribisha vijana wote walioteuliwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza Uzalendo, Umoja wa Kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na Utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.

 

Orodha kamili ya majina ya vijana, makambi ya JKT waliyopangiwa na vifaa wanavyotakiwa kuripoti navyo vinapatikana kwenye tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz

 

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,

Makao Makuu ya JKT,

Tarehe 08 June 2018.

 

 

 

Uadilifu

JKT huwajenga vijana kuwa waaminifu, wakweli na wakutegemewa na Taifa

Umoja na Mshikamano

Kuandaa vijana kuwa jamii yenye mshikamano na umoja wa kitaifa bila kujali itikadi zao za kitamaduni, kisiasa na kidini.

Kujitolea

Kuandaa vijana kuwa na moyo wa kujituma na kujitolea.

Uzalendo

Huwaandaa vijana wawe na moyo wa uzalendo, udugu na kuipenda nchi yao.

Nidhamu

Kuwafundisha vijana kuwa watiifu na wenye heshima.

Kupenda kazi

Kuwaanda vijana kuwa jamii yenye kutekeleza wajibu na moyo wa kupenda kufanya kazi