Jumatano, 03 Juni 2020

 

 

                                                                            

 

TAARIFA KWA UMMA

 

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limefanya uteuzi wa awamu ya pili ya wanafunzi waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita mwaka 2018 kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.

 

Vijana hao wanatakiwa kuripoti katika makambi ya JKT waliopangiwa kuanzia tarehe 14 Juni 2018 hadi tarehe 20 Juni 2018.

 

JKT linaendelea kusisitiza kuwa ni kosa la kisheria kwa mhitimu yoyote wa elimu ya kidato cha sita aliyeteuliwa kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria (Compulsory) kukaidi kuhudhuria mafunzo hayo.

 

Mkuu wa JKT anawakaribisha vijana wote walioteuliwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza Uzalendo, Umoja wa Kitaifa, stadi za kazi stadi za maisha na Utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.

 

Orodha kamili ya majina ya vijana walioteuliwa awamu ya kwanza na awamu ya pili, vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo na makambi waliyopangiwa vinapatikana kwenye tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz

 

BOFYA HAPA CHINI KUANGALIA MAJINA YA VIJANA WALIOCHAGULIWA MUJIBU AWAMU YA PILI 2018

 

 

BULOMBORA-KIGOMA       KANEMBWA-KIGOMA      MAFINGA-IRINGA

 

MARAMBA-TANGA              MGAMBO-TANGA             MLALE-RUVUMA

 

MSANGE-TABORA          MTABILA-KIGOMA          NACHINGWEA-LINDI

 

RWAMKOMA-MARA

 

 

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,

Makao Makuu ya JKT,

Tarehe 13 June 2018.

Uadilifu

JKT huwajenga vijana kuwa waaminifu, wakweli na wakutegemewa na Taifa

Umoja na Mshikamano

Kuandaa vijana kuwa jamii yenye mshikamano na umoja wa kitaifa bila kujali itikadi zao za kitamaduni, kisiasa na kidini.

Kujitolea

Kuandaa vijana kuwa na moyo wa kujituma na kujitolea.

Uzalendo

Huwaandaa vijana wawe na moyo wa uzalendo, udugu na kuipenda nchi yao.

Nidhamu

Kuwafundisha vijana kuwa watiifu na wenye heshima.

Kupenda kazi

Kuwaanda vijana kuwa jamii yenye kutekeleza wajibu na moyo wa kupenda kufanya kazi