Rais Mteule Dk John Pombe Magufuli
Rais Mteule Dk John Pombe Magufuli akionyesha cheti cha uteuzi wa kuwa Rais Mteule alichokabidhiwa na Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi Jaji Damian Lubuva, shughuli iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubelee, Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Akizindua Mradi wa huduma ya chakula Mafinga
Makamu wa Rais Dkt Mohammed Bilali (Watatu kutoka kulia) akizindua jengo la maradi wa huduma ya chakula na vyoo katika kijiji cha Idetero, Mafinga mkoani Iringa, wapli kutoka kulia ni Mkuu wa JKT Meja Jenerali Raphael Muhunga na wapili kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina Masenza.
Mafinga
Jengo la Mradi wa huduma ya chakula na vyoo katika kijiji cha idetero, Mafinga mkoani Iringa mbalo limezinduliwa na Mheshimiwa Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilali.
Mlalakuwa JKT
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda, akisalimiana
na Mkurugenzi wa Fedha Makao Makuu ya JKT, Kanali Kahema Mziray, alipotembelea
Makao Makuu ya jeshi hilo leo.
Mh Waziri Mkuu atembelea Makao Makuu JKT
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda, akizungumza na wajumbe wa Baraza la Taifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), hawapo pichani na watendaji wa JKT, katika
ukumbi wa jeshi hilo Makao Makuu ya JKT.
Pongwe-Msungura
Mkuuwa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Raphael Muhuga akimpokea Mheshiwa Raisi na Amiri Jeshi Mkuu Dk Jakaya Kikwete pamoja na Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi Dk husein Mwinyi katika uzinduzi wa mradi mpya wa uzalishaji wa kokoto unaoendeshwa na shirika la uzalishaji mali la SUMAJKT uliopo eneo la Pongwe Msungura tarehe 19 Oktoba 2015
Rais Kikwete azindua mradi wa uzalishaji kokoto
Raisi Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa mradi wa Kokoto wakati wa uzinduzi wa mradi huo tarehe 19 Oktoba 2015
Pongwe-Msungura
Kutoka Kushoto kwenda kulia, Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Job Masima , Mkuu wa Utawala na Mafunzo Brigedia Jenerali Jacob Kingu, Mkurugenzi wa Vocational Training Kanali Chacha Wanyancha, Mkurugenzi wa mahusiano JKT Kanali Zephan Marembo na Mkurugenzi wa Utumishi JKT Kanali Menas Mbele
Mradi wa uzalishaji wa kokoto
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua rasmi mradi wa kokoto Uliopo Pongwe Msungura unaoendeshwa na shirika la uzalishaji mali (SUMAJKT) tarehe 19 Oktoba 2015
Tengeru
Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yaUlinzi na Usalama Dkt Jakaya Kikwete (wa tano kulia)na Wakuu wa kamandi za JWTZ kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu –DULUTI Tengeru Jijini Arusha
Mafinga
Mkuu wa JKT Meja Jenerali Raphael Muhuga akikagua Gwaride la kumaliza kozi kwa vijana mujibu wa sheria Operesheni Kikwete kaika kikosi cha Mafinga JKT
Ruvu JKT
Mkuu wa Utawala na Mafunzo Brigedia Jenerali Jacob Kingu akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evaristo Ndikilo kwenye ofisi za Kamanda Kikosi Ruvu JKT muda mfupi kabla ya kufunga mafunzo ya vijana mujibu wa sheria OP Kikwete
Mafinga
Vijana wa JKT Mujibu wa Sheria Operesheni Kikwete katika kambi ya Mafinga JKT wakila kiapo muda mfupi kabla ya kufungwa mafunzo hayo.