Jumatatu, 23 Julai 2018
02 Sep
Rais atunuku Nishani

Rais atunuku Nishani

Mh Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jakaya Kikwete akimtunuku nishani Brigedia Jenerali Jacob Kingu wakati wa sherehe maalumu za kumuaga Mh Rais zilizofanyika Ikulu Dar es Salaam.

23 Mei
Utaratibu wa kujiunga na Jeshi la kujenga Taifa

Utaratibu wa kujiunga na Jeshi la kujenga Taifa

Awamu ya kwanza; vijana 20,000 wataripoti kwenye makambi ya mafunzo ya jkt kuanzia tarehe 01 juni 2014 na kuanza rasmi mafunzo yao tarehe 08 juni 2014 na kumaliza tarehe 04 septemba 2014. orodha yao itaanza kuonekana kwenye website ya jkt tarehe 11 mei 2014 kuanzia saa nne (4) asubuhi.

Awamu ya pili; vijana 14450 wataripoti kwenye makambi ya mafunzo ya jkt kuanzia tarehe 11 septemba 2014 na kuanza rasmi mafunzo tarehe 18 septemba 2014 na kumaliza tarehe 17 desemba 2014.

Orodha yao itaanza kuonekana kwenye website ya jkt tarehe 15 mei 2014 kuanzia saa kumi (10) jioni. Kijana yeyote mwenye ulemavu unaoonekana aripoti katika kambi ya mafunzo ya ruvu jkt (832 kikosi cha jeshi).

Vijana wote wanatakiwa kuwa na vyeti vya kumaliza kidato cha sita ( leaving certificate). Inasisitizwa vijana waripoti kwenye makambi waliopangiwa na sio kuja makao makuu ya JKT

Uadilifu

JKT huwajenga vijana kuwa waaminifu, wakweli na wakutegemewa na Taifa

Umoja na Mshikamano

Kuandaa vijana kuwa jamii yenye mshikamano na umoja wa kitaifa bila kujali itikadi zao za kitamaduni, kisiasa na kidini.

Kujitolea

Kuandaa vijana kuwa na moyo wa kujituma na kujitolea.

Uzalendo

Huwaandaa vijana wawe na moyo wa uzalendo, udugu na kuipenda nchi yao.

Nidhamu

Kuwafundisha vijana kuwa watiifu na wenye heshima.

Kupenda kazi

Kuwaanda vijana kuwa jamii yenye kutekeleza wajibu na moyo wa kupenda kufanya kazi