Jumatatu, 23 Julai 2018

MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, DKT John Magufuli, akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Martin Busungu, baada kumaliza hotuba kwenye kituo cha Uwekezaji Mgulani JKT, Machi 18 mwaka huu.

Uadilifu

JKT huwajenga vijana kuwa waaminifu, wakweli na wakutegemewa na Taifa

Umoja na Mshikamano

Kuandaa vijana kuwa jamii yenye mshikamano na umoja wa kitaifa bila kujali itikadi zao za kitamaduni, kisiasa na kidini.

Kujitolea

Kuandaa vijana kuwa na moyo wa kujituma na kujitolea.

Uzalendo

Huwaandaa vijana wawe na moyo wa uzalendo, udugu na kuipenda nchi yao.

Nidhamu

Kuwafundisha vijana kuwa watiifu na wenye heshima.

Kupenda kazi

Kuwaanda vijana kuwa jamii yenye kutekeleza wajibu na moyo wa kupenda kufanya kazi