Jumanne, 23 Oktoba 2018

. Featured

 

 

Vijana wa Kujitolea Operesheni Magufuli wa Kambi ya Mtabila JKT Mkoani Kigoma wakifanya Mtihani wa mwisho wa Stadi za Kazi na Stadi za Maisha leo tarehe 11 October 2018. Vijana watakaofaulu watapatiwa Vyeti vya kuhitimu Masomo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Mtihani huo wa Masomo nane (8) unaofanywa na Vijana wa Operesheni Magufuli waliopo katika Makambi ya JKT nchini, Wameanza tarehe 09 October 2018 na wanamaliza leo tarehe 11 October 2018. Picha hapo juu. 

Uadilifu

JKT huwajenga vijana kuwa waaminifu, wakweli na wakutegemewa na Taifa

Umoja na Mshikamano

Kuandaa vijana kuwa jamii yenye mshikamano na umoja wa kitaifa bila kujali itikadi zao za kitamaduni, kisiasa na kidini.

Kujitolea

Kuandaa vijana kuwa na moyo wa kujituma na kujitolea.

Uzalendo

Huwaandaa vijana wawe na moyo wa uzalendo, udugu na kuipenda nchi yao.

Nidhamu

Kuwafundisha vijana kuwa watiifu na wenye heshima.

Kupenda kazi

Kuwaanda vijana kuwa jamii yenye kutekeleza wajibu na moyo wa kupenda kufanya kazi