Jumatano, 14 Novemba 2018

. Featured

Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe.Dkt Hussein Mwinyi ametembelea Mkoa wa Singida na kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi pamoja na jengo la Mkuu wa Mkoa ambapo limegharimuTshs 499 Milioni, ukarabati majengo ya Hospitali Tshs 77 Milioni, ujenzi wa majengo ya kuhifadhia Maiti, kufulia nguo na kulia chakula Tshs 1.1 Bilion ambapo miradi yote hiyo inatarajiwa kukabidhiwa Desember 2018. Katika ziara hiyo Mhe Waziri Mwinyi anaambatana na Mkuu wa JKT Meja Jenerali Martin Busungu na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Kanali Rajabu Mabele.

Uadilifu

JKT huwajenga vijana kuwa waaminifu, wakweli na wakutegemewa na Taifa

Umoja na Mshikamano

Kuandaa vijana kuwa jamii yenye mshikamano na umoja wa kitaifa bila kujali itikadi zao za kitamaduni, kisiasa na kidini.

Kujitolea

Kuandaa vijana kuwa na moyo wa kujituma na kujitolea.

Uzalendo

Huwaandaa vijana wawe na moyo wa uzalendo, udugu na kuipenda nchi yao.

Nidhamu

Kuwafundisha vijana kuwa watiifu na wenye heshima.

Kupenda kazi

Kuwaanda vijana kuwa jamii yenye kutekeleza wajibu na moyo wa kupenda kufanya kazi