Jumanne, 11 Desemba 2018

. Featured

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na JKT, Mhe.Dkt Florens Turuka akiweka jiwe la msingi la ukumbi wa burudani la kikosi alipokuwa kwenye ziara yake ktaika Kikosi cha Chita JKT Mkoani Morogoro. Katika ziara hiyo Katibu Mkuu ameambatana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT anayeshughulikia operesheni za kibiashara, Luteni Kanali Peter Lushika. Picha hapo juu.

Uadilifu

JKT huwajenga vijana kuwa waaminifu, wakweli na wakutegemewa na Taifa

Umoja na Mshikamano

Kuandaa vijana kuwa jamii yenye mshikamano na umoja wa kitaifa bila kujali itikadi zao za kitamaduni, kisiasa na kidini.

Kujitolea

Kuandaa vijana kuwa na moyo wa kujituma na kujitolea.

Uzalendo

Huwaandaa vijana wawe na moyo wa uzalendo, udugu na kuipenda nchi yao.

Nidhamu

Kuwafundisha vijana kuwa watiifu na wenye heshima.

Kupenda kazi

Kuwaanda vijana kuwa jamii yenye kutekeleza wajibu na moyo wa kupenda kufanya kazi