Jeshi la Kujenga Taifa

 • Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa
  Meja Jenerali Muhuga akila kiapo kuwa mkuu mpya wa Jeshi la Kujenga Taifa
 • 2
  Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali SA Ndomba na Mnadhimu Mkuu mstaafu Luteni Jenerali Shimbo wakiwa na Mkuu mpya wa JKT
 • Mke wa Waziri Mkuu
  Rais Kikwete akiwa na Mnadhimu Mkuu Luteni Jenerali Ndomba pamoja na Mkuu mpya wa JKT Meja Jenerali Muhuga
 • kikwete rais
  Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Na Usalama Na Rais, Dkt. Jakaya Kikwete, akipokea zawadi ya saa ikiwa na picha yake kutoka kwa Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Raphael Muhuga, alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo Mlalakuwa jijini Dar es Salaam.
 • kikwete rais 1
  Dkt. Jakaya Kikwete, akisalimiana na wanadhamimu wakuu wa kada mbalimbali alipokuwa akiwasili katika Uwanja wa Makao Makuu ya JKT (MMJKT) kuzungumza na maafisa, askari na watumishi wa umma.
 • mafunzo1
  Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania, Dr Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Mkuu wa JKT na washiriki wa kwanza katika mafunzo ya JKT.
 • mafunzo2
  Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa wakitoa salamu ya heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu Dr Jakaya Mrisho Kikwete katika maadhimisho ya Miaka 50 ya Jeshi hilo.
 • mafunzo11
  Moja ya mavazi yaliyokuwa yakitumiwa na Jeshi la Kujenga Taifa.

 

 

 

HABARI MBALIMBALI

TANGAZO


MABADILIKO YA TAREHE YA KURIPOTI MAFUNZO YA VIJANA MUJIBU WA SHERIA SEPTEMBA 2014

MAJINA YA WALIMU NGAZI YA DIPLOMA 2014 MUJIBU WA SHERIA NA VIKOSI WALIVYOPANGIWA WATAKAORIPOTI KUANZIA TAREHE 04SEPTEMBA

MAJINA YA WALIMU NGAZI YA CHETI 2014 MUJIBU WA SHERIA NA VIKOSI WALIVYOPANGIWA WATAKAO RIPOTI KUANZIA TAREHE 04 SEPTEMBA..

MAJINA YA VIJANA KIDATO CHA SITA 2014 MUJIBU WA SHERIA AWAMU YA PILI NA VIKOSI WALIVYOPANGIWA..

 

 

 

 

 

 

Meja Jenerali
Raphael Muhuga

Mkuu wa JKT na SUMAJKT

Mawasiliano na
Jeshi la Kujenga Taifa

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa
S.L.P 1694, Dar es salaam

Simu:+255-22-2780588/2780712
Fax:+255-2-270048
Email: info@jkt.go.tz

Website:www.jkt.go.tz


 

 

 

 

 

JESHI LA KUJENGA TAIFA

Moja ya vyombo vilivyoundwa na Serikali ya Tanganyika mara tu baada ya Taifa hili kupata uhuru ni Jeshi la Kujenga Taifa na lililoasisiwa tarehe 10 Jul 1963. Jeshi la Kujenga Taifa au kwa kifupi JKT, liliundwa ili kuponya majeraha yaliyoachwa na serikali ya kikoloni miongoni mwa jamii ya watanzania ambayo ni pamoja na ubaguzi miongoni mwao katika misingi ya kidini, makabila, rangi na kipato. Chombo hiki ni muhimu katika kuelimisha na kuandaa vijana wa kitanzania kiuzalendo, kimaadili, kinidhamu na kuwafanya raia wema wanaopenda kutumikia na kulinda nchi yao.

Vikosi vya JKT ni mahali ambapo vijana hupata fursa ya kujifunza kikamilifu na kwa vitendo, maana na umuhimu wa kazi na pia kujifunza kutoa huduma kwa Taifa lao bila kutegemea kulipwa ujira wowote. Kwa hiyo, imedhihirika wazi ya kuwa wajibu wa JKT katika maendeleo ya Taifa hili ni mkubwa na muhimu sana.

Nchi mbalimbali duniani zina taasisi zinazofanana na taasisi yetu ya JKT. Kwa msingi huo nchi yetu kuwa na JKT ni jambo la kujivunia sana. JKT vilevile ni chombo cha kujenga Umoja na Utaifa kwa vijana wetu.

Dira

Kupitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa, hatimaye Tanzania iwe ni jamii yenye nidhamu, umoja, uzalendo, undugu, wakakamavu na kupenda kazi.

Dhima

Kuwalea vijana wa Tanzania, kinidhamu, uzalendo, ukakamavu na kuwafundisha ujuzi na hatimaye kuchangia katika ulinzi wa Taifa na maendeleo ya kiuchumi.

Gazeti la Vijana Leo

Historia ya JKT

Barua pepe

SHUGHULI MBALIMBALI ZA JESHI LA KUJENGA TAIFA