TAARIFA KWA UMMA
KUSITISHWA KWA MAFUNZO YA JKT KUNDI LA KUJITOLEA KWA MWAKA 2020/2021
Jeshi la Kujenga Taifa linapenda Kuutaarifu Umma kuwa Mafunzo ya JKT kwa Kujitolea kwa mwaka 2020/2021 yaliyokuwa yaanze hivi karibuni katika makambi mbalimbali nchini, Mafunzo hayo yamesitishwa kwa muda mpaka hapo itakavyotangazwa.
Kutokana na Kusitishwa kwa mafunzo hayo, JKT linawataka Vijana wote ambao walichaguliwa na kuripoti makambini kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Kujitolea, Warejee majumbani kwao, na wale ambao walikuwa bado hawajaripoti wasiende kuripoti katika makambi waliyopangiwa mpaka hapo itakapotangazwa tena.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,
Makao Makuu ya JKT,
Tarehe 19 Januari 2021.