TAARIFA KWA UMMA
WITO WA KURIPOTI MAKAMBI YA JESHI LA KUJENGA TAIFA.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge, Anautaarifu Umma kuripoti makambini Vijana waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya JKT kwa Kujitolea kwa mwaka 2020/2021 ambao Mwezi Februari 2021 walirejeshwa majumbani.
Vijana wanaotakiwa kuripoti makambi ya JKT waliyokuwa wamepangiwa hapo awali ni wale wenye Elimu ya darasa la Saba na Elimu ya kidato cha nne. Waripoti makambini kuanzia tarehe 7 Mei hadi tarehe 14 Mei 2021.
Vijana wenye Elimu ya Kidato cha Sita, Ngazi ya Cheti, Stashahada, Shahada na wale wenye Taaluma ya Uhandisi wataendelea kusubiri majumbani hadi hapo utaratibu mwingine utakapotangazwa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,
Makao Makuu ya JKT,
Tarehe 30 April 2021.