Tanzania emblem
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

JESHI LA KUJENGA TAIFA -JKT

JKT ENDELEENI KUFANYA KAZI KWA BIDII

15 May, 2022
JKT ENDELEENI KUFANYA KAZI KWA BIDII

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Mhe. Dkt Stergomena Tax, amewataka Maafisa, Askari, vijana na Watumishi wa Umma kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo ya kuanzish-wa kwa Jeshi la kujenga Taifa.

Waziri Stagomena Tax ametoa kauli hiyo leo Makao Makuu ya JKT Chamwino mkoani Dodoma katika ziara yake ya kwanza kutembelea Kamandi ya JKT tangu kuteuliwa kwake kushika wadhifa huo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Amesema ameridhishwa na kupongeza mafanikio makubwa yaliyofikiwa na JKT hasa katika malezi ya vijana ambalo ni jukumu mama sanjari na usimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia Shirika la Uzalishajimali (SUMAJKT).

Aidha amewataka vijana wa JKT kulitumikia Taifa lao na kuweza kujitegemea kupitia mafunzo mbalimbali wanayopatiwa na Jeshi hilo wakati wa mafunzo.Sanjari na hilo amewataka vijana hao pia kuviishi viapo vyao kwa kudumisha nidhamu, uadilifu na kufanya kazi kwa bidii.