Tanzania emblem
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

JESHI LA KUJENGA TAIFA -JKT

Majukumu ya Jeshi la Kujenga Taifa

MAJUKUMU YA MSINGI( Objectives)

1. Malezi ya Vijana

 • Vijana kufundishwa moyo wa kupendana bila kujali tofauti za itikadi, dini, kabila na kipato.
 • Kupenda kazi za mikono.
 • Kuthamini na kuendeleza mila, desturi na kudumisha utamaduni wa Taifa.
 • Kuwa raia wema, wanaojiamini, wanaojituma, wenye uzalendo na kuipenda nchi yao.

2.Ulinzi wa Taifa

 • Kuwapa vijana mbinu za kijeshi wawe Jeshi la akiba, kuwaandaa vijana watakaofaa kujiunga na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.
 • Kuwaandaa vijana kusaidia katika majanga mbalimbali, mfano mafuriko, moto na ajali mbali mbali.

3.Uzalishaji Mali

 • Ili kuwafanya vijana wa kitanzania waepukane na kusumba kuwa kazi za ofisini ndio njia pekee na bora inayomuwezesha mtu kuishi, JKT linahusika na uzalishaji mali kwa lengo la kuwawezesha vijana kujiajiri katika sekta mbali mbali mara baada ya kumaliza mkataba na JKT. Uzalishaji mali unaofanywa na JKT ni pamoja na:-
 • Kujenga na kukarabati majengo
 • Viwanda na Kilimo
 • Madini na Nishati
 • Utalii
 • Ulinzi kwa Taasisi binafsi (Security Guard Services)
 • Maduka (Super Market)
 • Kuunganisha magari na mitambo
 • Huduma za elimu