Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe. Dkt. Stergomena Tax (katikati) akijionea uzalishaji wa mahindi kwenye Shamba Darasa la JKT, alipotembelea Banda la Jeshi la Kujenga Taifa katika Maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni, Dodoma.
Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe. Dkt. Stergomena Tax, akiangalia bidhaa ya Maji Safi ya kunywa aina ya Uhuru peak yanayozalishwa na kiwanda cha SUMAJKT Bottling Company, alipotembelea Banda la JKT kwenye Maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni, Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera akijionea uzalishaji wa bidhaa za ngozi unaofanywa na kiwanda cha SUMAJKT SHOES & LEATHER PRODUCT, alipotembelea Banda la JKT katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni, Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera (katikati) akijionea uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na malighafi za kilimo alipotembelea Banda la JKT katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni, Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Thomas Cornel (aliyenyoosha mkono) akijionea samani zinazozalishwa na Kiwanda cha Chang’ombe JKT Furniture, alipotembelea Banda la JKT katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni, Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mhe. Thomas Cornel (wa pili kulia) akipata maelezo kuhusu baadhi ya mazao yanayozalishwa alipotembelea Banda la JKT katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni, Dodoma.
Moja ya vyombo vilivyoundwa na Serikali ya Tanganyika mara tu baada ya Taifa hili kupata uhuru ni Jeshi la Kujenga Taifa lililoasisiwa tarehe 10 Jul 1... Soma zaidi
Dira
Kupitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa, hatimaye Tanzania iwe ni jamii yenye nidhamu, umoja, uzalendo , undugu, ukakamavu na kupenda kazi.
Dhima
Kuwalea vijana wa Tanzania, ili kuwajengea nidhamu, uzalendo, ukakamavu na kuwafundisha ujuzi hatimaye kuchangia katika ulinzi wa Taifa na maendeleo ya kiuchumi