Tanzania emblem
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

JESHI LA KUJENGA TAIFA -JKT

KATIBU MKUU KILIMO AWATAKA JKT KULIMA MBEGU BORA

15 May, 2022
KATIBU MKUU KILIMO AWATAKA JKT KULIMA MBEGU BORA

Katibu Mkuu  Wizara ya  Kilimo, Mhe. Andrew Massawe amewataka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuendelea ku-tekeleza kwa vitendo azma ya kufanya kilimo cha mbegu bora sambamba na kuendeleza ujenzi wa miundo mbinu ya Umwagiliaji. Mhe. Massawe ametoa kauli hiyo akiwa ameambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na JKT Mhe. Dkt. Faraji Mnyepe mwishoni mwa wiki walipofanya ziara ya kikazi katika Shamba la SUMAJKT Mngeta Plantation Limited pamoja na Kikosi cha Chita JKT  Wilayani  Kilombero mkoani Morogoro.

Ameongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo inayo mikakati mikubwa katika kuwezesha kukamilika kwa ujen-zi wa miundo mbinu ya  Kilimo cha Umwagiliaji nchini katika maeneo makubwa matatu  Chita JKT, Rufiji na Kata-vi. "Binafsi nimefurahi sana baada ya kuona namna mlivyo serious na Kilimo, hivyo niahidi kuwa Serikali itaongeza nguvu katika kukamilisha mradi huu".

Alisema Mhe. Mas-sawe Ameongeza kuwa, Ili miradi hiyo ilete tija iliyokusudiwa, Ametembea na Wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo, Mku-rugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Ndg. Ray-mond Mndolwa ambaye atasaidia kufanikisha kukamilika kwa Ujenzi wa Miundo mbinu hiyo kwa ubora unaotaki-wa. Akizungumzia hitajio la Mbegu Bora nchini , Mhe. Mas-sawe amewataka JKT na SUMAJKT kutumia mashamba yao makubwa kuzalisha kwa wingi mbegu  bora za mazao mbalimbali pamoja na kufanya kilimo cha  Soya kwani soko lake ni kubwa ndani na nje ya Nchi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Faraji Mnyepe amesema JKT imeanza  kutekeleza kwa vitendo sera ya kilimo biashara kwa kufanya kilimo cha mbegu bora. Aidha alimshukuru Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo kwa kutenga muda wake na kutembelea shughuli zinazofany-wa na JKT pamoja na SUMAJKT mkoani humo.

Nae Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema JKT litayafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na wa-taalamu yenye lengo la kuboresha shughuli za kilimo kikosini hapo. "Tunashukuru sana wataalam ambao umeambatana nao katika ziara hii kwani wametuelekeza na kutushauri katika namna ya kuboresha ili kuweza kufikia malengo ya mradi huu". Alisema Meja Jenerali Mabele