Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini Congo (DRC) Meja Jenerali Kasongo Kabwik akipokea zawadi ya jozi ya kiatu (buti) toka kwa Mkuu wa Tawi la Utawala JKT nchini Brigedia Jenerali Hassan Mabena zinazotengenezwa katika Kiwanda cha bidhaa za ngozi kinachomilikiwa na JKT kilichopo Mlalakuwa jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride maalum la JKT lililoandaliwa kwa ajili yake kwenye kilele cha Maadhimisho ya jeshi hilo kutimizi miaka 60 toka kuanzishwa kwake lililofanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Vijana wa JKT wakipita mbele ya Jukwaa Kuu kwa mwendo wa haraka na kutoa heshima mbele ya Mgeni Rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya JKT toka kuanzishwa kwake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha miaka 60 ya JKT kwenye kilele cha Maadhimisho ya Jeshi hilo yaliyofanyika Julai 10, katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma
Rais Mtaafu wa Awamu ya Nne Mhe Dkt Jakaya Kikwete kushoto akiwaongoza Viongozi wa Serikali na Kijeshi pamoja na wananchi katika kushiriki JKT Marathon iliyofanyika Jijini Dodoma.
Moja ya vyombo vilivyoundwa na Serikali ya Tanganyika mara tu baada ya Taifa hili kupata uhuru ni Jeshi la Kujenga Taifa lililoasisiwa tarehe 10 Jul 1... Soma zaidi
Dira
Kupitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa, hatimaye Tanzania iwe ni jamii yenye nidhamu, umoja, uzalendo , undugu, ukakamavu na kupenda kazi.
Dhima
Kuwalea vijana wa Tanzania, ili kuwajengea nidhamu, uzalendo, ukakamavu na kuwafundisha ujuzi hatimaye kuchangia katika ulinzi wa Taifa na maendeleo ya kiuchumi